Fahamu

Mwenyekiti wa mtaa auawa akisuluhisha ugomvi usiku wa manane

Familia ya laani kitendo cha ndugu yao ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Mashariki (CCM), Kata ya Nyamanoro Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza Kijungu Oraka Magesi anayedaiwa kuuwawa wakati akitimiza majukumu yake.

Mwenyekiti huyo inadaiwa kuchomwa kisu kwenye mbavu upande wa kushoto Mei 29, 2020 usiku wa saa 8 hadi 9 na mmoja wa wananchi wa mtaa huo wakati alipokwenda nyumbani kwake kusikiliza na kusuluhuisha kesi.

Kwa mujibu wa NIPASHE, Akizungumza kwa niaba ya familia wakati wakuaga mwili wa marehemu huyo, Juma Kisero, amesema ni kweli binadamu tunazaliwa na tunakufa na kifo ni mipango ya Mungu lakini vifo vingene vinaumiza hasa kama hicho kilichomtokea ndugu yao kinasikitisha.

“Vifo vingine pamoja na kuwa ni mipango ya Mungu lakini vinaumiza sana, kijana wangu huyu ambaye siku hiyo alirudi nyumbani salama kutoka kwenye majukumu yake lakini usiku wake akaitwa na mmoja wa wananchi ambaye alikua ana shida na wakati anatimiza majukumu yake  ndipo mauti yalipo mkuta,lakini najiuliza mtu usiku anaenda kusuluhisha kesi alafu anachomwa kisu sina majibu ya kujiridhisha na muachia Mungu tu,” amesema Kisero.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa (A), Amini Fataki akielezea tukio hilo amesema kama wenyeviti ambao ni viongozi wa wananchi kwa ngazi ya mitaa wamesikitishwa na kulaani kitendo hicho kilicho mtokea kiongozi mwenzao na kusababisha mauti.

“Ili kuwa ni siku ya Ijumaa usiku wa kuamkia Jumamosi mnamo mida ya saa nane kwenda saa tisa usiku, alifuatwa nyumbani kwake na wadada wawili ambao walitaka msaada wake, kwani mtu huyo aliyemchoma kisu alikuwa amempiga mmoja kati ya wadada hao wawili na alikua amegoma kutoka kufungua mlango kwa madai mpaka Mwenyekiti huyo aende,” ameeleza Fataki.

Kwa mujibu wa Fataki, amesema baada ya hapo aliiaga familia yake na kufika eneo la tukio na akawauliza baadhi ya majirani waliokuwa wametoka nje kama wanamfahamu wakajibu ndio,ndipo alipogonga mlango kwa mtuhumiwa na kujitambulisha pia na alipotoka nje alitoka na kisu na kumchoma nacho Mwenyekiti huyo kwenye mbavu upande wa kushoto karibu na titi.

Amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alipelekwa Polisi huku Mwenyekiti huyo pamoja na dada aliyekuwa amepigwa walipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Sekou-Toure kwa ajili ya matibabu ambapo ilikua siku alfajili ya Jumamosi lakini kwa bahati mbaya ilipofika mida ya saa mbili usiku mei 30 mwaka huu alifariki.

Source Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents