Tupo Nawe

Mwigulu ataja mbinu za ushindi wa CCM, Afunguka wakurugenzi kusimamia uchaguzi ‘Hata wapinzani mkisimamia tutashinda’

Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba (CCM) ameeleza sababu tano za kwanini chama chake cha CCM kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zote kubwa zilizowahi au zinazofanyika sasa hivi.

Mwigulu Nchemba

Mwigulu Nchemba kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa ushindi ambao wamekuwa wakiupata Chama Cha Mapinduzi hautokani na kupendelewa na Wakurugenzi ambao ni wasimamizi wa uchaguzi, bali ni kutokana na historia ya chama hicho.

Kwa upande, mwingine Nchemba amezungumzia hukumu ya mahakama kuhusu wakurugenzi kutosimamia uchaguzi, ambapo amesema vyama vya upinzani waache kutafuta huruma wawaache wanasheria wafanye kazi zao kuhusu kesi hiyo.

ACT & CO USHINDI WA CCM HAUTOKANI NA HISANI YA WAKURUGENZI BALI KWA KURA ZA WANANCHI.
1)CCM inaheshima ya Urithi wa UKOMBOZI WA NCHI HII ambayo chama kingine chochote hakina.

2) CCM inamtandao wa wanachama na muundo wa KITAASISI KULIKO chama chochote kile hapa nchini.

3) CCM mara zote imekuwa na ILANI BORA, SERA BORA na Wagombea BORA KULIKO chama chochote kile.

4) CCM IMEFANYA KAZI NZURI KUPITIA SERIKALI ZAKE YA KULETA MAENDELEO NCHINI NA INAAMINIWA NA WANANCHI KULIKO CHAMA CHOCHOTE KILE.

5) ACHENI WANASHERIA WAFANYE YA KISHERIA, WANASIASA MSITAFUTE HURUMA/VISINGIZIO WAKATI WENGINE HAMNA HATA WANACHAMA WANAOFIKIA IDADI YA WACHAMA WA CCM WA KWENYE KIJIJI KIMOJA. “HATA ACT & Co MSIMAMIE WENYEWE UCHAGUZI, CCM INA WAPIGA KURA, ITASHINDA …TUKUTANE SITE”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW