Mwigulu Nchemba apokelewa kifalme jimboni kwake, amshukuru Rais Magufuli kwa kumpumzisha (+picha)

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba mkoani Singida Dkt. Mwigulu Nchemba amejitokeza kwa mara ya kwanza hadharani jimboni kwake tangu asimamishwe kazi na Rais Magufuli.

Mwigulu Nchemba

Mwigulu kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema amefanya mkutano na wananchi wa jimbo lake na kumshukuru Rais Magufuli kwa kumpumzisha kwani uongozi ni kupokezana.

Nimefanya mkutano na wananchi jimboni Iramba, kushukuru chama changu CCM na Mh. Rais kwa nafasi aliyonipa ya utumishi.Uongozi ni kupokezana kijiti. Nawashukuru pia Wanairamba kwa mkutano mzuri,Sasa nitakuwa na muda mwingi zaidi wa kufuatilia miradi ya maendeleo ya jimbo langu hususani utekelezaji wa ilani ya CCM na shughuli mbalimbali za serikali.“ameandika Mwigulu Mchemba.

Mwigulu Nchemba alitenguliwa nafasi ya uwaziri na Rais Magufuli wiki iliyopita soma zaidi-Rais Magufuli amtumbua Waziri Mwigulu Nchemba, amtaja atakayechukua nafasi yake

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW