Habari

Mwili wa Akwilina kuagwa chuo cha NIT Mabibo

Mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline unatarajiwa kuagwa February 22 katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu amesema baada ya kuaga mwili huyo siku ya Alhamisi, atazikwa mkoani Kilimanjaro Februari 23, 2018.

Akwilina aliyefariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema

“Tutamuaga ndugu yetu siku ya Alhamisi katika viwanja vya chuo cha NIT pale Mabibo na siku hiyo hiyo tutaanza safari kuelekea Rombo-Mashati Olele mkoani Kilimanjaro na mazishi tutafanya Ijumaa,” amesema Kiyeyeu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents