Michezo

Mwili wa Cheick Tiote wawasili Ivory Coast kwa Mazishi (Picha+Video)

Mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Cost na klabu ya Beijing Enterprises ya China, Cheick Tiote wawasili Ivory Coast kwaajili ya mazishi.

Tiote, ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji waliyoiwezesha timu ya taifa ya Ivory Cost kushinda taji la michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2015 alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya China.

Familia ya mwanasoka huyo ilikuwa inahitaji mazishi yake yafanyike nyumbani kwao Yamoussoukro lakini Shirikisho la soka la Ivory Coast limetangaza kufanyika mjini Abidjan.

Maelfu ya watu akiwemo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Cost, Herve Renard waliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abidjan kuupokea mwili wa Tiote siku ya Jana.

Wachezaji kama, Kolo Toure, Gervinho pamoja na Siake Tiene walikuwepo katika kuupokea mwili mwili huo
Toure, amemuelezea mchezaji huyo aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Newcastle United kuwa alikuwa mchezaji mwenye kiwango bora.

Cheick Tiote amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30.

Picha na Video za matukio baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Cost


BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents