DStv Inogilee!

Mwili wa Kofi Annan kuzikwa leo Accra, Ghana 

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan unatarajiwa kuzikwa hii leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Kofi Annan

Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi kadhaa wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Machifu, wanasiasa na jamaa wanaonekana wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa Kofi Anna katika lango la kuingia ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Accra Jumatano

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.

Leo inahitimisha kilele cha wiki kadhaa ya maandalizi ya mazishi yake, ambaye ni mmoja wa wana diplomasia wanaoheshimika duniani.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra anasema kuwa, ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Wachezaji ngoma wa jamii ya Ashanti wakati wa ibada iliyofanyika Jumatano

Miongoni mwa waombolezaji hao ambaye tayari amewasili mjini humo ni aliyewahi kuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela, Bibi Graca Machel.

Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Ivory Coast, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria shughuli hizo za mazishi, wakiwemo pia marais wa zamani kutoka nchi za Ujerumani, Finland na Uswizi

Shughuli hizo za kumuaga marehemu zitafuatiwa na mazishi yatakayofanywa kwa ndugu wa karibu na kwa heshima zote za kijeshi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW