Habari

Mwili wa mama mzazi P Funk Majani kuzikwa Uholanzi

Mwili wa mama mzazi wa mtayrishaji wa muziki wa BongoFleva P Funk Majani, Aunt Sheilah umeshindikana kurudi ili kuzikwa Tanzania kwa sababu ya changamoto ya usafiri na Ugonjwa wa Corona, hivyo unatarajiwa kuzikwa leo nchini Uholanzi.

Producer P Funk Majani, na marehemu Mama yake

Mwenyekiti wa kamati wa maandalizi wa msiba huo ambaye ni msanii Soggydogg Anter, amesema mwili utazikwa Uholanzi na P Funk mwenyewe yupo huko kwa ajili ya mazishi, ambapo atarejea Tanzania Ijumaa usiku na siku ya Jumamosi watafanya dua maalum kwa marehemu.

Siku ya leo tunatarajia mwili wa mama mzazi wa P Funk Majani Aunt Sheilah kuzikwa nchini Uholanzi, imebidi azikwe huko kwa sababu usafiri ulikuwa mgumu na wenzetu bado wana wasiwasi na ugonjwa wa Corona, P Funk Majani mwenyewe tayari yupo huko kwa ajili ya mazishi na atarejea Tanzania siku ya Ijumaa usiku, kisha Jumamosi itafanyika dua ya marehemu nyumbani kwake Bamaga mahali ambapo ipo studio za Bongo Records” amesema Soggydoggy Anter

Mama wa P Funk Majani alifariki nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu siku ya Septemba 8, na taarifa kuhusu kifo chake zilitoka Tanzania siku ya Septemba 10.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents