Aisee DSTV!

Mwili wa mtoto wakutwa makaburini ukiwa umeharibika vibaya, Fahamu zaidi

Mwili wa mtoto wakutwa makaburini ukiwa umeharibika vibaya, Fahamu zaidi

Mwili wa mtoto anayefahamika kwa jina la Kelvin Stephano (12), umeokotwa katika makaburi yaliyopo mtaa wa Nsemulwa kwa Mkumbo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ukiwa umekwishaharibika.

Picha ya makaburi

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Rashid Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kutokana na mwili wa marehemu kuharibika vibaya, haikuweza kubainika moja kwa moja  chanzo cha kifo chake.

Kwa upande wake Stephano Robart Makofia, ambaye ni mzazi wa marehemu amesema, alipofika eneo la tukio alimtambua mtoto wake kwa mavazi aliyokuwa amevaa siku aliyotoweka nyumbani.

Kwa mujibu Eatv majirani wameitupia lawama familia hiyo, kwa madai walikuwa hawamjali mtoto wao.

Aidha Kamanda wa Polisi ametoa Rai kwa wazazi mkoani Katavi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka majanga kama hayo kuwakuta watoto.

Chanzo Eatv https://www.eatv.tv/news/current-affairs/katavi-mwili-wa-mtoto-wakutwa-makaburini

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW