Habari

Mwili wa mwanasiasa Kenya wapatikana mtoni

By  | 

Mwili wa mwanasiasa Thomas Minito, kutokea nchini Kenya wapatikana ukielea katika mto karibia na mji wa Machakos, kilomita hamsini mashariki mwa Nairobi.

Mwanasiasa huyo alikamatwa na polisi March 30 mwaka huu, kwa kuchochea vurugu na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari, Kuki Gallmann ambaye aliuwawa kwa kupigwa na risasi.

Polisi nchini Kenya wanasema mwanasiasa Minito alijihusisha na uvamizi wa mashamba ya kibinafsi, na amepatikana ameuawa. Walimtambua kupitia stakabadhi zilizokuwa mfukoni mwake. Polisi katika mji wa Laikipia -Kenya wanaendelea kuwasaka waliovamia mashamba mbalimbali eneo hilo. Hii ni baada ya wafugaji kuvamia mashamba ya watu binafsi wakitafuta lishe.

Hata hivyo familia yake bado haijadhibitisha kifo cha mwanasiasa huyo.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments