Burudani

Mwili wangu ndio biashara yangu – Calisah (+video)

By  | Mwanamitindo anayekuja kwa kasi nchini Tanzania, Calisah amesema kwa sasa anajifua na mazoezi ili kuutengeneza mwili wake uwe wa kibiashara zaidi kwa ili uvutie watu wanaotaka kufanya nae kazi za matangazo.

Calisah

Hata hivyo, Calisah amesema kuwa kitendo cha yeye kupata matangazo mengi na kuonekana kwenye mabango kinamfanya ajiweke vizuri kwa kufanya mazoezi ili awe na muonekano wa kijasiri huku akikataa kuwa hafanyi mazoezi kwa ajili ya kupendwa na mademu.

Mimi biashara yangu ni mwili wangu kama ambavyo ukiuza nguo mtaji wako ni nguo, Mgari magari ukiuza gari lazima u-invest kwenye magari mengine, mimi kazi yangu ni Modo watu wamezoea kuniona kwenye Tv kwenye mabango kwenye runway hivyo lazima nijiweke fiti“,amesema Calisah kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Kwa upande mwingine Mwanamitindo huyo amesema kuwa mwaka huu ameamua kuachana na fani hiyo ya mitindo na kuingia kwenye masumbwi.

 

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments