Mwingine Zaidi Apata Dhamana EPA

IDADI ya watuhumiwa waliopata dhamana jana ilifikia 13 baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Madai cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Esther Komu kuachiwa kwa dhamana baada ya kuwasilisha hati ya mali yenye thamani ya Sh450

IDADI ya watuhumiwa waliopata dhamana jana ilifikia 13 baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Madai cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Esther Komu kuachiwa kwa dhamana baada ya kuwasilisha hati ya mali yenye thamani ya Sh450 milioni kama dhamana.
Mpaka sasa idadi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambao wameshaachiwa huru kwa dhamana, imefikia 13 baada ya mfanyakazi huyo wa BoT kukamilisha masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama na kuachiwa huru.
Komu na wafanyakazi wenzake watatu wanakabiliwa na kosa la kufanya uzembe na kuisababishia BoT hasara ya Sh 2.2 bilioni.

Katika kesi hiyo namba 1162 wameunganishwa na wafanyabiashara wengine wawili, Rajabu Maranda ambaye anadaiwa kuwa ni kada wa CCM mkoani Kigoma, na mwenzake Farijala Hussein ambao ndio walioiba pesa hizo baada ya kuidhinishiwa na wafanyakazi hao.

Komu alipata dhamana hiyo mbele Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa kwa niaba ya Hakimu Mkazi Warialwande Lema, anayesikiliza kesi hiyo, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali yenye thamani ya Sh 450 milioni kupitia kwa wakili wake Mabere Marando, kama moja ya masharti ya dhamana.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wote watano kwa pamoja wanatakiwa kuweka fedha taslimu ama hati ya mali yenye thamani sawa na nusu ya kiasi cha fedha wanachodaiwa kuiba, ambacho ni sawa na Sh1.1bilioni kwa mtindo wa kugawana sawa kiasi hicho kwa watuhumiwa wote ambapo kila mmoja anapaswa kutoa kiasi kama hicho alichokitoa Komu.

Wafanyakazi wengine wawili wa BoT katika kesi hiyo ni pamoja na Sophia Joseph, ambaye alipata dhamana juzi, na Iman Mwakosya ambaye bado yuko mahabusu.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents