Mwinjuma adai aliitosa Twanga Pepeta baada ya mmiliki kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba

Mwimbaji na mtunzi mahiri wa muziki wa dance nchini Mwinjuma Muumini amesema aliamua kuachana na bendi kongwe ya Twanga Pepeta kutokana na mmiliki wa bendi hiyo kushindwa kutimiza matakwa katika mkataba wao.

muumini

Akiongea na Star TV, Muumini amesema hiyo ndio sababu kubwa ya kwanini waimbaji kama yeye huhama bendi mara kwa mara.

Alisema licha ya kutangaza kuwa hatoihama bendi hiyo, alilazimika kuondoka baada ya mmiliki wake Asha Baraka kushindwa kutimiza ahadi alizokuwa amempa.”Mimi nilipanga nyumba ya milioni mbili kwa mwaka na bosi wa Twanga aliniahidi kuwa atakuwa akiniongeza laki sita lakini sikupata hiyo hela ndio maana nilifikia wakati nikaamua kuhama,” alisema Muumini.

Kwa sasa muimbaji huyo amejiunga na bendi ya Victoria Sound inayoundwa pia na Waziri Sonyo pamoja na waimbaji wengine.

Mwinjuma Muumini alitamba sana miaka kadhaa iliyopita na utunzi wa nyimbo kama Tunda akiwa na Tamtam Sound iliyokuwa inamilikiwa na ASET, na baadae kuihama bendi hiyo na kuzunguka kwenye bendi tofauti tofauti ambapo mwaka jana aliamua kurudi kwenye kampuni ya ASET na kujiunga na Bendi ya African Stars,

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents