Habari

Mwinyi aonya kuhusu ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa nchini

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amesema licha ya kupatikana kwa maendeleo katika miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara na maendeleo ya demokrasia yaliyopatikana bado nchi inakabiliwa na tatizo la kuweka mbele maslahi binafsi kwa baadhi ya wanasiasa.

ali-hassan-mwinyi
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na TBC1, Mzee Mwinyi amesema ubinafsi unaathiri maendeleo ya taifa.

“Vyombo vyetu vya siasa visiwe sababu ya sisi kukosana, kuna baadhi ya watu eeh mtu haruhusiwi kumuoa mchumba wake kwasababu wazazi wake hawataki kwasababu huyu mchumba wake si mwenzetu, tunaingilia mpaka uhuru wa mtu na uhuru wa roho yake,uhuru wa nafsi yake, uhuru wa moyo wake, tunafika hadi kwasababu ya siasa, tupende nchi yetu tupende vyama vyetu lakini visiingilie uhuru na matakwa ya watoto wetu na ndugu zetu wenyewe,” alisema Mwinyi.

“Lakini jambo la watu wengi linapendwa hivyo hivyo na watu wengi mara nyingi mnakuta mnapata mashindano makubwa makubwa mnazozana na kwakuwa watu wako wengi mnadhamiri vilevile mkiwa watu wengi na nia huwa nyingi. Kuna watu wengine wanataka mambo yawe bora kwa wengine na wengine wanataka mambo yawe bora kwa yeye mwenyewe. Ikiwa hivi kwangu itakuwa bora kuliko kwa hivi vinginevyo hapa ndipo tunapopata matatizo.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents