DStv Inogilee!

Mwinyi wa Machozi Band na Wema Sepetu wavalishana Pete kimovie zaidi

Wema Sepetu katika kurekodi movie yake mpya ya Superstar itakayozinduliwa mwezi wa sita mwaka huu, ameamua kutumia sehemu za maisha yake na kurudia kuzirekodi ili kuweza kuitumia katika story ndani movie yake hiyo.

Movie hiyo iliyoanza kurekodiwa machi mwaka huu itagusia maisha anayoishi Wema Sepetu na kuwaonyesha watu mazuri na mabaya ya kuwepo kwenye industry kwa jinsi yeye anavyoyaona kila siku ya maisha yake. Wema ambaye alirekodi scene ya kuvishwa pete na Mwinyi Goha ndani ya new Maisha Club aliamua kurudia kama ile ya Diamond akimvisha yeye pete na Mwinyi kutumia maneno yale yale ya Diamond ili mradi kunogesha movie yake mpya.

Wema amekanusha kwa watu kwamba Mwinyi ni mchumba wake na kuweka wazi ni kazi ya kisanaa zaidi iliyopelekea kwa wao kuvishana pete hiyo usiku wa jana.

pics courtesy of Bongo Star Link

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW