Michezo

Mwinyi Zahera wa Yanga amgaragaza Patrick Aussems na makocha wengine ligi kuu

Kamati ya tuzo za Wachezaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL),  imeanzisha tuzo mpya ya kocha bora wa mwezi itakayokuwa inatolewa kila mwezi kwa lengo la kutambua mchango wa kocha husika katika ligi hiyo.

kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ‘Mkongoman’

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati hiyo imemtangaza kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ‘Mkongoman’ kuwa kocha bora wa mwezi uliyopita wa Septemba na kuwaacha wenzake wa ligi kuu patupu akiwemo wa Simba, Patrick Aussems.

Kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems

Zahera ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameonekana akimwaga mshindani wake wa karibu, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji  anayeiongoza klabu ya Simba na mameneja wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa mwizi uliyopita.

Hata hivyo kamati hiyo ya tuzo imemtangaza, Amri Said wa Mbao FC kuwa kocha bora wa mwezi Agosti hii ni kwa mujibu wa taarifa za TFF zilizotolewa leo hii.

Kwa upande mwingine Ofisa Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface wambura amesema kamati ya saa 72 itakutana muda wowote ili kujadili matukio ya utovu wa nidhamu yaliyojitokeza katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.

Wachezaji Pascal Wawa, Herieter Makambo, Andrew Vicent na James Kotei ambao wameonekana kupitia vipande vya video ‘video clips’ zilizosambaa mitandaoni wakijihusisha na vitendo visivyo vya kiungwana watajadiliwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

”Hizi ‘video clips’ zinazotembea mitandaoni ndizo zinazotukutanisha ila siwezi kuzungumzia hatua zitakazo chukuliwa hadi kamati tutakapokutana,”amesema Wambura.

Tayari mshambuliaji wa Simba John Bocco amezuiwa kucheza michezo mitatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumpiga ngumi beki wa Mwadui ya Shinyanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents