Habari

Mwisho back Home

Mshiriki katika shindani la Big Brother All Stars kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba aliwasili nchini jana na kupokelewa na baba yake  mzazi pamoja na ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere.

Mwisho alilakiwa kwa kupewa shada la  maua akitokea Afrika Kusini ambako alikuwa kati ya tano bora kwenye shindano hilo la  Big bother All star Africa  2010.

Wawakilishi wa  kampuni ya Multchoice Tanzania walikuwepo katika msafara huo wa kumpokea Mwisho kwani wao ndio Kampuni mama ya Mnet Africa walioratibu na kuendesha mashindano hayo.

Ingawa Mwisho hakupata bahati ya kushinda dola laki mbili, alijipatia mchumba, mshiriki mwenzake kutoka Namibia, Meryl.

Mwisho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Bongo5 na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Big Brother na habari kuwahusu washiriki wenzake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents