Burudani

Mwisho Mwampamba akabiliwa na ubaguzi wa hali ya juu nchini Namibia

Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania mara mbili kwenye shindano la Big Brother Africa, Mwisho Mwampamba amesema amekuwa akikumbana na ubaguzi wa hali ya juu nchini Namibia ambako anaishi na mke wake Meryl Shikwambane aliyekuwa mshiriki mwenzie wa BBA.

149_31004415600_5978_n

Mwampamba ameshare kupitia Facebook jinsi anavyokumbana na ubaguzi huo.

“Kwakuwa sasa Namibia ipo huru naona woga dhidi ya raia wa kigeni (xenophobia) imekuja kwa kasi. Polisi walikuja nyumbani kwangu na kuniambia natakiwa nirudi kwenye nchi yangu. Manyanyaso kwenye mpaka. Huwa napata visa ya miezi miwili tu licha ya kuwa SADC na nimeoa Mnamibia. Swali langu ni, maveterani wenu wote wametoka wapi? Mnawatendea wakoloni wenu wa zamani vizuri kuliko wakombozi wenu? Huwa inafedhehesha kuona jinsi Wanamibia na wa Afrika Kusini walivyo.

Wanamibia na Waafrika Kusini wanatutendea sisi Waafrika wengine kama nyani kwakuwa sasa mko huru. Wamesahau mapema jinsi tulivyowasaidia japokuwa tulikuwa maskini na wenye njaa. Ni sawa, tulifanya sababu kilikuwa ni kitu sahihi kufanya na si kupata fadhila yenu. Lakini tunatarajia walau heshima na kutendewa kama binadamu,” aliandika Mwisho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents