Michezo

Mwl Kashasha achambua CV ya kocha mpya Simba na uwezo wake ”Patrick Aussems hajafeli, tuliyofeli ni sisi” (+Audio)

Mchambuzi mahiri wa mchezo wa soka hapa nchini, Mwalimu Alex Kashasha amemchambua Kocha Mpya wa klabu ya Simba,Sven Vanderbroeck huku hakusita kumwagia sifa Patrick Aussems ambaye ametimuliwa kazi na timu hiyo hivi karibu.

”Tumpe muda tuone, muda utazungumza, Simba aliwahi kuja Profesa lakini aliondoka. Makocha waliyo kuja hapa licha ya CV za makaratasi wamekuja hapa kwa rekodi zao.” Amesema Kashasha

Mwalimu Kashasha ameongeza kuwa ”Wakija hapa kinatokea nini ?, alikuja Profesa hapa alikuwa Simba, alikuwa George Lwandamia kutoka Zambia kutokea Zesco kili tokea nini, aliondoka hapa na mpaka anaondoka yalisemwa mengi.”

”Alikuwepo Zahera hapa juzi, akiwa kocha msaidi wa timu ya taifa ya DR Congo, moja ya timu kubwa Barani Afrika, kimetokea nini kwa Zahera ?.”

”Aussems alikuwa haja shindwa, alifaanya timu imekuwa kwenye ubora wake mpaka anaondoka, timu ilikuwa inacheza mpira mzuri, inaongoza ligi, imepoteza mechi moja na kudroo moja wakati wenzao wanapigwa asubuhi na jioni.”

”Kwa nini unaamini kwenye timu 20, lazima Simba awe wa kwanza, kwa nini kwasababu timu nyingi zinachea ligi, zina wataalamu waliosoma vyuo tofauti, waliocheza mpira na uzoefu tofauti.”

”Kwa nini timu ikifungwa muamini kwamba nyinyi hamstaili kufungwa kwa nini mnaingia kwenye ushandani. Timu zenye majina zikifungwa zinatafuta mchawi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents