Habari

Mwongozo wa kutafuta kazi inayoendana na malengo yako

Kama unatafuta kazi, soma HAPA upate dondoo chache zinazoweza kukusaidia, na kukuongezea kwa zile ulizonazo tayari,

1. Unatakiwa ujue wapi unaangalia au kutafuta kazi

Hapa inamaanisha usitumetume barua zako za kuomba kazi popote. Fanya uchunguzi na uelewe ni makampuni gani yanahitaji watu kama wewe na je unawezaje kuingia huko? Unaweza ukasema hicho kitu hakiwezekani ila ukweli ni kwamba kinawezekana, ni wewe kuhakikisha mipango yako na namna unavyofuatilia uwe na uhakika na watu unaowasiliana nao.

Kama una ujuzi sahihi na umejikita kwa umakini na umadhubuti mkubwa haitakuwia vigumu kupata kazi sehemu sahihi na yenye malengo yako ya muda mrefu au mfupi.

2. Linganisha malengo yako na maadili ya kikazi na maisha yako binafsi

Watu wengi hushindwa kuchukua malengo yao binafsi na kuoanisha na kazi wanazokwenda kufanya. Kabla ya kuomba kazi au kuingia mkataba unahitaji kujua malengo ya kampuni hiyo au taasisi hiyo na wawe wanaajili watu wenye mwelekeo wao.

Ni vizuri kwa wewe kujitambua vizuri kabla ya kuingia huko ili uweze kuendana nao. Usipofanya hivyo utajikuta unakuwa na wakati mgumu sana kama malengo yako na ya kwao ni tofauti kabisa. Mfano kama unaingia kwenye taasisi ambayo maadili ya kazi ni mazuri na wewe maadili yako ni ya kubabaisha utajikuta unapata shida vivyo hivyo kama maadili yako ni mazuri halafu ukaingia kwenye taasisi ambayo haina maadili utapata shida na hata kuhahatarisha maisha yako.

3. Unahitaji kuonyesha uwezo na ujuzi wako kikamilifu

Utakapokuwa umepata taasisi au kazi inayokufaa unahitaji kuwafanya wajue uwepo wako kwa utofauti wako na ubunifu wako. Makampuni mengi hayaogopi watu ambao wanaonyesha umahiri wao kazini, hivyo wanakuhitaji sana ufanye kitu cha tofauti kuliko wengine katika uwezo, ujuzi na utendaji wako.

Kuna vitu vingi ambavyo tunaviamini ambavyo kwa wakati mwingine vimeathiri taaluma zetu. Huu ni wakati wa kubadilika katika mawazo na utendaji wetu ili kuhimili katika soko la ajira lenye changamoto na ushindani mkubwa.

Unahitajika kuwa ni mtu asiye na lawama au mlalamikaji bali uwe mtu ambaye utaweza kusaidia kampuni kuleta majibu ya bidhaa au huduma wanayotoa kwa ubunifu wa hali ya juu sana. Kuna vitu vingi unavijua na namna ambavyo vinatakiwa kufanyika kwa usahihi, chukua hatua madhubuti na kufanya kwa usahihi hii itakusaidia kuwa huru ndani ya nafsi yako mwenyewe na kukuongezea heshima kwenye kazi yako na watu amabao unafanya nao kazi.

Usipuuzie maadili yako ambayo unayathamini kwa kiasi kikubwa kwa gharama yoyote ili kuweza kuridhisha watu wengine Ni vizuri ukajiweka kando kuliko kuharibu taaluma yako kimaadili. Hii ndio maana unatakiwa kuchunguza kwa usahihi ni wapi unakwenda kufanya kazi na kwanini? Kumbuka kuwa maisha yako ya baadaye yatasomwa kulingana na kile unachokifanya sasa, utavuna ulichopanda.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents