Burudani

Mzazi mwenzake na Zari afariki dunia

By  | 

Mzazi mwenzake na Zari The Bosslady, Ivan Ssemwanga amefariki dunia katika hospitali nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo.

Ivan ambaye alifanikiwa kupata watoto watatu na Zari, baby mama wa Diamond Platnumz, alikimbizwa hospitalini mapema wiki iliyopita baada ya kupoteza fahamu. Kupitia mtandao wa Instagram, Zari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kuweka picha ya bosi huyo na kuandika ujumbe wa kusikitisha.

“God loves those that are special and that’s exactly who you were & I guess that’s why he wanted you to himself. You have touched and helped thousands, you did wonders and I remember you telling me “life is too short let me live it to the fullest”, this very dark hour it makes sense why you always said those words to me,” ameandika Zari.

“To your sons, you were a hero-some kind of superman. Anyone who has ever been in your presence knows what a charming person you were. You will be missed and remembered in so many ways. You were IVAN THE GREAT! Rest in peace DON,” ameongeza.

Sisi kama Bongo5 tunatoa pole kwa msiba huo na tunamuombea kwa Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments