Tupo Nawe

Mzee Afanyiwa sherehe baada ya kupotea kwa miaka 51, asimulia ilivyokuwa – Video

Mzee Afanyiwa sherehe baada ya kupotea kwa miaka 51, asimulia ilivyokuwa - Video

Mzee wa miaka 81 aitwaye Francis Muthua Chege, amerudi nyumbani baada ya kupotea kwa miaka 51 akiwaacha mke wake na watoto sita katika kijiji cha Ikumbi nchini Kenya.

Mzee Francis Muthua Chege.

Mzee huyo aliiacha familia yake mwaka 1968 wakati huo akiwa ana umri wa miaka 30 na kutokomea katika misitu ya Mau, ila hakumwambia mke wake na watoto wapi anaelekea.

Baada ya kurudi nyumbani Mzee huyo aliwasimulia watu, ndugu, jamaa na marafiki vitu alivyokuwa anafanya baada ya kutoweka kwa miaka 51.

“Nilikuwa nauza mkaa kisha fedha zote ambazo napata zinatumika kununua pombe. Mke wangu wa pili na mtoto wetu wa kiume walishindwa kuvumilia tabia yangu na wakaamua kuodoka. Niliishi katika masikitiko makubwa na hata kuhofia kurejea nyumbani mikono mitupu,” amesimulia Francis Muthua Chege.

Ameongeza kusema alikuwa hana hata nauli ya kurudi kijijini kwao ndipo alipoenda katika kituo cha polisi kuomba msaada kupata nauli kurudi kijijini alipotoka.

Baada ya kurejea kijijini kwao wanafamilia waliandaa karamu fupi ya chakula na vinywaji wakisheherekea tukio la kurudi kwake baada ya muda mrefu.

Chanzo Daily Nation.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW