Michezo

Mzee Akilimali ashusha dua zito kabla ya kuikabili Simba ”Yaarabbi Yaarabbi turudishie umoja”

Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya watani zao Simba SC kunahaja ya kutupilia mbali tofauti zao na kumuomba Mungu katika kuhakikisha wanachomoza na ushindi siku hiyo ya Aprili 29.

Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali

Wakati zimesalia siku mbili pekee kabla ya kukutana kwa watani hao wajadi Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye dimba la Taifa siku ya Jumapili hii, Mzee Akilimali ametumia muda wake kuiyombea timu yake kuhakikisha inachomoza na ushindi siku hiyo.

Tunalengo la kuwashinda wapinzani wetu, siyo rahisi lakini lazima ujiandae kwa hayo wazee tunatoa baraka zote kwa vijana kwakuwa hatuna kinyongo.

Isipokuwa mimi naomba tu Yaarabbi Yaarabbi nakuomba turudishie hali yetu ileile ya umoja na mshikamano wetu kwa kila hali, tushikamane kwaajili ya kuwasapato vijana wetu na tumuombe Mwenyezi Mungu kila mmoja kwa dua yake na imani yake ili tupate ushindi siku hiyo ya Jumapili.

Nawaomba wana Yanga wenzangu tuwe wamoja tuwache tofauti zetu twende katika mchezo maana ni mgumu sana.

Kocha mpya ameingia na viongozi wetu wamefanya mambo haraka haraka sasa hivi yupo kazini, Msimbazi ubingwa bado isipokuwa tu mtu hawezi kukata tamaa ila hali bado. Amenitambuka mechi chache tu na yeye atarajie kufanya vibaya kwenye mechi hizo alizo nazo.

Wazee hatuna ahadi yoyote kwa vijana kwakuwa hayo yanatamkwa na viongozi.

Simba ambayo inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 59 nyuma ya hasimu wake Yanga wenye alama 48 zinatarajia kukutana siku ya Jumapili ya Aprili 29 kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents