Michezo

Mzee Kilomoni awatolea uvivu wapinzani wao ”Yanga watakiona chamtema kuni”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni ametamba kuwa atawafunga wapinzani wao Yanga SC kwenye mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara utakao pigwa Aprili 29 siku ya Jumapili.

Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni

Mzee Akilimali ashusha dua zito kabla ya kuikabili Simba ”Yaarabbi Yaarabbi turudishie umoja”

Mzee Kilomoni amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu wamewaandalia dozi wapinzani wao na kukiona cha mtama kuni.

Mech ya Jumapili itakuwa ngumu kwa sababu Simba na Yanga ni timu kubwa katika nchi hii, kwahiyo ni mchezo mgumu lakini tutafanya vizuri.

Mazungumzo hayakosekani kuelekea kwenye mechi ya Simba na Yanga, lakini Yanga watakiona chamtama kuni ,tumewaandalia dozi utacheza na Yanga bila kuwaandalia dozi.

Tumewaandalia dozi ya Ujerumani watacheza marimba sisi tutacheza soka ninapocheza na Yanga jeuri lazima iwepo nawaambia wana Simba waje tu kwa wingi kuishabikia timu yao.

Niwakati wetu huu wa kuchukua ubingwa utakaaje miaka minne bila kunyakuwa taji.

Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents