Bongo Movie

Mzee Majuto apata ahueni baada ya kuugua ghafla

Mchekeshaji King Majuto baada ya kulazwa hospitali kwa muda wa siku tatu , ameruhusiwa na kurudi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji wa hernia (ngiri) mkoani Tanga.

Mke wa muigizaji huyo, Bi. Aisha Majuto amesema kwamba tatizo lililokuwa likimsumbua mumewe lilianza siku nyingi ingawa kwa wiki iliyopita hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi hadi kufikia kulazwa.

“Ni kweli tulikuwa tumelazwa lakini mume wangu amesharuhusiwa na kurudi nyumbani. Tatizo ni hernia (ngiri) na ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri ingawa hawezi kuzungumza kwa muda mrefu”, Bi Aisha Majuto.

Hata hivyo mama huyo amesema utachua muda kidogo mpaka muigizaji huyo arudi tena katika kazi yake ya kuigiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents