Habari

Mzee mwingine anayetibu kwa kikombe kama babu wa Loliondo aibuka Dar

Mamia ya watu wa jiji la Dar es salaam jana Septemba 13, 2018 wamemiminika katika eneo la Feri kupata tiba baada ya mtu mmoja aliyeibuka na kutangaza kuwa anagawa dawa ya asili ambayo inatibu maradhi yote.

Jacob Kawawa

Mganga huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jacob Kawawa ameliambia gazeti la Nipashe kuwa anauza dawa hiyo kwa Tsh 3,000/= na vipimo vyake ni tofauti na vile vya mzee wa Samunge ambaye alikuwa anatumia kikombe.

Kawawa amesema yeye anatumia chupa ya maji ya lita moja, ambapo mpaka sasa watu wenye maradhi mbalimbali ikiwemo kisukari, kansa na magonjwa mengine wameshapona kabisa, kupitia tiba yake.

Mashuhuda walioongea na gazeti la Nipashe, wamesema kuwa Mganga huyo alianza kutoa tiba hiyo katika eneo la Feri mwezi mmoja uliopita na hakupata wateja wengi, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda wateja wanazidi kuongezeka na wengine wakitoa ushuhuda.

Chanzo – https://www.ippmedia.com/sw/habari/mzee-mwingine-wa-kikombe-aibuka-dar

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents