Habari

Mzee Mwinyi atoa neno kuhusu amani ya nchi

Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema amani ni uhai wa nchi na wananchi pasipo na amani ni vigumu hata kufikiri mambo yatakavyokuwa.

Mzee Mwinyi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa dini, uliofanyika jijini Dar es salaam na kuandaliwa na Kamati ya Amani mkoani humo.

“Viongozi wa dini wamefundisha amani, wameilea amani katika mzunguko mzima wa maisha. Pia wameunda majukwaa kwa ajili ya kuienzi amani, amesema Mzee Mwinyi”.

Mwinyi amesema Tanzania kama sehemu ya jamii ya kimataifa inaishi katika uhalisia wakuwepo katika dini mbalimbali na kwa miaka mingi imejulikana kama kisiwa cha amani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents