Michezo

Mzee Mwinyi mgeni rasmi Simba SC Vs Gendarmerie Nationale FC

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo amesema kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya timu Gendarmerie Nationale FC siku ya Jumapili.

Kwenye mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Simba SC, Manara amesema “Tunategemea kuwa Mzee wetu, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mchezo wetu dhidi ya Gendarmerie Nationale FC kwenye michuano ya kombe la shirikisho la CAF , mchezo huu ambao utachezwa Jumapili saa 10:00 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,” amesema Manara.

Kikosi cha Gendarmerie Nationale FC kinatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi majira ya saa 7:00 usiku kikitokea Djibouti kikiwa ni msafara wa watu 18 na viongozi nane.

Viingilio vya mchezo huo vitakuwa ni 30,000 kwa VIP A, 20,000 VIP B, Orange 10,000 na 5,000 kwa mzunguko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents