Mzee Ruksa Kupanda Mlima Kilimanjaro

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alli Hassan Mwenyi a.k.a Mzee Ruksa, Jumamosi ijayo ataongoza ujumbe wa watu 55 wakiwemo wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Geita (GGM), kupanda Mlima Kilimanjaro kwa muda wa siku sita.

mwinyi_1.jpg

 

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alli Hassan Mwenyi a.k.a Mzee Ruksa, Jumamosi ijayo ataongoza ujumbe wa watu 55 wakiwemo wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Geita (GGM), kupanda Mlima Kilimanjaro kwa muda wa siku sita.

Tukio hilo ni la kwanza la kihistoria kwa kiongozi wa juu wa aina ya Mwinyi kupanda mlima huo ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya gonjwa hatari la ukimwi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika kumuaga Mzee Mwinyi kuanza safari hiyo kuelekea kilele cha Uhuru, akifuatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk James Nsekela.

Kilele cha Uhuru cha Mlima Kilimanjaro kina urefu wa mita 5,698 kutoka usawa wa bahari. Mzee Ruksa amenukuliwa katika taarifa hiyo akisema kuwa

“Naingia katika changamoto hii si kwa sababu nataka kuwashinda wengine au kuweka historia, bali kuchangisha fedha za mapambano ya ukimwi, nawaomba watu mbalimbali na mashirika wajitokeze kunifadhili na kuniunga mkono kwa sababu kwa njia hiyo safari yangu hii ya kupanda mlima Kilimanjaro itakuwa na manufaa makubwa” alisisitiza Mwinyi.

Mzee Mwinyi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 83, mwaka jana aliwaomba waandaaji wa tukio hilo wamuunganishe kuwa miongoni mwa watu watakaopanda mlima huo mwaka huu.

Senkoro alisema wameamua kupanda mlima huo kupitia njia ya Machame ambayo ni ngumu na yenye baridi kali kwa kuwa hata mapambano dhidi ya ukimwi nayo ni magumu kama ilivyo kupanda mlima huo kupitia Machame.

Makampuni mbalimbali yamejitokeza kufadhili safari hiyo ikiwamo AngloGold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya GGM, kampuni ya simu za mkononi ya Celtel Tanzania, Barrick Gold, Mantrac, Komatsu, Atlas Copco, Sandvik na African Explosives.

Mengine ni Benki za Stanbic na NBC, Rhino Lodge of Ngorongoro, hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, All Terrain Services (ATS), New Africa Hotel, Coastal Travel and Tours na Zara Tours ya mjini Moshi.

Hadi kufikia wiki iliyopita, ahadi za michango kwa ajili ya kuchangia tukio la mwaka huu linalojulikana kama Kilimanjaro Challenge Against HIV/AID ilikuwa imefikia Dola za Marekani 231,000 ambazo ni sawa na karibu Sh260 milioni. Tangu kuanzishwa kwa mpango huo na GGM mwaka 2002, zaidi ya Sh995milioni zimechangwa na wadau mbalimbali ambazo zilipelekwa kusaidia watoto yatima, wajane na taasisi zinazojishuhulisha na vita dhidi ya ukimwi.

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents