AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Mzee Yusuf ajiimarisha kibiashara, anunua Scania ya mizigo na kufungua kiwanda (Picha)

Aliyekuwa muimbaji wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuf ameendelea kujiimarisha zaidi kibiashara baada ya siku za hivi karibuni kufungua kiwanda chake kidogo cha kusaga unga pamoja na kununu gari kubwa aina ya Scania kwaajili ya kubebea bidhaa zake.

“Welcome home my baby boy. Alhamdulillah,” aliandika Mzee Yusuf baada ya kuonyesha gari hiyo.

Mzee Yusuf awali alikuwa muimbaji wa muziki wa taarab mwenye mafanikio makubwa zaidi na baadae aliachana na masuala hayo na kuamua kujiingiza kwenye dini.

Awali alianza na biashara ya matofali na baadaye ufugaji ambao ulimwendea vizuri na kumjengea umaarufu huyo Chanika jijini Dar es salaam.

Wiki hii kupitia Instagram yake alishare biashara yake hiyo mpya kwa mashabiki kama unavyoona hapo juu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW