Burudani

Mzee Yusuph kuongeza mke wa tatu?

Muimbaji wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph huenda akaoa mke wa tatu hivi karibuni.

mzee2
Mzee Yusuph akiwa na mke wake mkubwa Leila

Tayari muimbaji huyo ana wake wawili, Leila Rashid na Chiku ambao inasemekana wakiwa hawapatani hata kidogo kiasi cha kurushiana vijembe katika mitandao.

Mzee Yusuph amethibisha mpango huo kupita U Heard ya XXL, Clouds FM.

Amedai kuwa wivu ni jambo la kawaida na hashangai kuona wake zake wakipigana vijembe. Mzee Yusuph amesema kuongeza mke mwingine huenda ikawa dawa ya wake zake hao na kwamba hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa nao.

mzee4
Mzee Yusuph akiwa na mke wake mdogo Chiku

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents