Michezo

Mzimu wa Coutinho kuitafuna Liverpool

Mkurugenzi mkuu wazamani wa klabu ya Liverpool, Christian Purslow amesema huwenda timu hiyo ikampoteza meneja wake, Jurgen Klopp na kujiunga na moja kati ya wapinzani wao wakubwa endapo watashindwa kutimiza malengo ya Mjerumani huyo.

Hayo yamekuja baada ya Liverpool kumuuza kiungo wake, Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa gharama ya paundi milioni 145 mwishoni mwa wikiendi hii hivyo, Purslow anaamini the Reds watalazimika sasa kutumia fedha hizo kufanya usajili utakao leta tija ndani ya kikosi hicho.

“Nashindwa kufahamu hasa kwa nini wanashindwa kufanya usajili utakaokuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi kama wameweza kumuuza mchezaji kwa gharama kubwa,”amesema Purslow ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa klabu ya Liverpool mwaka 2009 na 2010.

“Ninahakika, Jurgen Klopp bilashaka atakwenda kuwa kocha kati ya moja ya klabu kubwa na hasimu wa Liverpool kama watashindwa kumtimizia malengo yake.”

Klabu za Manchester na Chelsea huwalinda wachezaji wao na kutoruhusu kuwapoteza kirahisi ni tofauti ukilinganisha na Liverpool, Arsenal na Tottenham Hotspur kwa mujibu wa Purslow.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents