Habari

Mzozo wa Iran na Marekani: Trump asema yuko tayari kuzungumza, adai mipango ya kuishambulia ilikuwa tayari atoa sababu za kutofanya hivyo

Rais wa taifa kubwa duniani, Trump amesema kuwa haitaji vita lakini ameiyonya Iran kuwa itakabiliwa na makosa ya “uharibifu” vita vikizuka. Akizungumza na kituo cha habari cha NBC siku ya Ijumaa, amesema Marekani iko tayari kwa mazungumzo lakini haitakubali Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Televisheni ya Iran imeonesha picha ya kile inachosema ni mabaki ya ndege ya Marekani isokuwa na rubani

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Pia alizungumzia kwa kina kwanini alisitisha mashambulizi dhidi ya Iran dakika za mwisho kujibu hatua ya taifa hilo kudungua ndege yake isokuwa na rubani wiki hii, akisema aliambiwa raia 150 wa Iran wangeliuawa.

“Sikupendela hatua hio. Sidhani ni sawa kufanya hivyo,” alisema. Tehran Inasema ndege ya Marekani ambayo haikuwa na rubani iliingia anga lake mapema siku ya Alhamisi. Marekani inasisitiza kuwa ndge hiyo ilikuwa ikipaa juu ya anga la kimataifa.

Hali ya taharuki imekuwa ikiongezeka kati ya mataifa hayo mawili, huku Marekani ikiilaumu Iran kwa kushambulia meli za mafuta zinazohudumu katika eneo hilo.A handout photo made available by the US Navy provided by Northrop Grumman, a RQ-4 Global Hawk unmanned aerial vehicle conducts tests over Naval Air Station Patuxent River, Maryland, USA 25 June 2010

Iran ilidungua ndege aina ya RQ-4A Global Hawkya jeshi la majini la Marekani (file photo)

Irana imetangaza kuwa hivi karibuni itazidisha kiwango cha kimataifa kinachodhibiti uzalishaji wa madini ya Uranium katika mpango wake wa nyuklia.

Mwaka Jana rais Trump alijiondoa katika Mkataba wa Kimataifa wa wa nuklia uliofikiwa mwaka 2015 iliyokuwa na lengo la kudhibiti shughuli za nyuklia za Iran.

Marekani sasa imeiomba kukutana na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kujadili hatua ya Iran.

Trump aliiambia nini NBC?

Alisema mpango wa kuishambulia Iran”ilikuwa tayari na ilikuwa inasubiri amri yake” lakini alipoambiwa na majenerali wake ni watu wangapi watauawa katika shambulizi hilo akasitisha hatua hiyo.

“Niliwaza kwa sekunde moja hivi , kisha nikawaambia, mnajua nini, wao wameangusha ndege isiokuwa na rubani sisi tukiamua kulipiza kisasi tutawaangamiza watu 150,” aliiambia NBC.

Alikanusha madai kuwa ndege zake tayari zilikuwa njiani kuelekea Iran kwa oparesheni hiyo – akisema: “Hakuna ndege ilikua angani.”

Bw. Trump alimwambia rais wa Iran: “Huwezi kumiliki silaha za nuklia,Nakama unataka tujadiliane kuhusu hilo ni sawa. La sivyo utaendelea kukabiliwa na vikwazo vya kiuchumi.”

Hatua ya Trump imechukuliwaje ?

Spika wa bunge Nancy Pelosi anasema alishukuru kuwa rais hakuchukua hatua ya kuishambulia Iran na kuongeza kuwa ni vyema wakati mwingine awasilishe ombi bungeni kabla ya kuchukua hatua ya kijeshi.

Baadhi ya vyombo vya Habari nchini Marekani vimeripoti kuwa shambulizi hilo lilikuwa limeidhinishwa na Pentagon, huku vingine vikiripoti kuwa maafisa wakuu wa Pentagon walikuwa wameonya kuwa hatua hiyo ingelihararisha hali ya vikosi vya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.A screenshot from Iran's Press TV purportedly shows the launch of an Iranian surface-to-air missile to shoot down the US drone

Iranimetoa kanda ya vido inayoonesha jinsi ilivyoishambulia ndege ya Marekani

Wazri wa mambo ya nje wa wa Marekani Mike Pompeo na mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama John Bolton walikuwa wameshikilia misimamo mikali kuhusiana na suala hilo lakini waliombwa na viongozi wengine nchini humo kuwa makini, Gazeti la Associated Press liliripoti.

Mamlaka ya usafiri wa angani nchini Marekani (FAA) imetoa agizo la kuzuia mashirika ya ndege ya marekani kupaa juu ya angaa la ghuba ya Uajemi na Oman.

Huku hayo yakijiri Mashirika kadhaa ya ndege yamefutilia mbali safari zao au kujiepusha na anga la Iran baada ya ndege ya ujasusi ya Marekani isiokuwa na rubani kudunguliwa na majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo.

Hiini baada ya ran kuthibitisha kuwa iliangusha ndege hiyo ikisema kuwa ilikiuka sheria za anga lake- japo Marekani inapinga madai hayo.

Ni ndege zipi zilizobzdili mkondo wa safari?

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, haya ndio mashirika ya ndege yaliobadilisha njia za ya ndege zao:

  • Cathay Pacific
  • Emirates
  • FlyDubai
  • British Airways
  • KLM
  • Qantas
  • Singapore Airlines
  • Lufthansa

Iran imesemaje?

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Iran ameonya kuwa mashambulizi yoyotedhidi ya “itakuwa na athari ya kimataifa”.

“Mlikiuka sheria za anga la Iran,nasisi tukajilinda,” Seyed Sajjadpour, mmoja wa manaibu wa wiziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo aliiambia, BBC.

He also said it was clear that there were members of Donald Trump’s administration who were intent on overthrowing Iran’s government.

Presentational grey line

Uchambuzi wa mwandishi wa BBC wa masuala ya ulinzi

Hatua ya Rais Trump kusitisha kuishambulia Iran imetuma ujumbe mkali kwa Tehran.

Mataifa hayo yalikaribia kuzua mzozo mkubwa wa kimataifa. Lakini katika mchezo huu wa kupimana nguvu, baadhi ya wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanahoji hatua hiyo ya Marekani just what message imepokelewa vipi na viongozi wa Iran?

Lakini wanasema Iran nayo kwa upande wao inaamini imetoa onyo kali kwa Marekani hasa kwa ndege zake za upelelezi zisizokuwa na rubani zinazoingia katika anga lake bila idhini.

Hatari kubwa hata hivyo ni ikiwa Iran itachanganywa na ujumbe usiokuwa wazi ikiwa mzozo kati yake na Marekani utasuluhishwa au la.

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran imeathiri vibaya sekta ya mafuta ya taifa hilo.

Na hatua ya Iran kuangusha ndege hiyo ya Marekani huenda ikazidisha uhasama kati ya mataifa hayo mawili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents