Burudani

Mzungu Kichaa aelezea mpango wa kuchukua uraia wa Tanzania

Msanii wa muziki mwenye asili ya Denmark, Mzungu Kichaa amesema ametamani mara kadhaa kutaka kuchuku uraia wa Tanzania lakini ameshindwa kufanya hivyo kutokana na aina ya uraia unaotolewa hapa nchini.

Mzungu Kichaa

Muimbaji huyo aliyezaliwa nchini Denmark na kukulia Tanzania alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV kuwa katika kazi yake ya sanaa anapenda kuwakilisha Tanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili pamoja na muziki wa Bongo Flava.

“Mimi naimba Kiswahili na Kiingereza kidogo, nimefikiria kubadilisha uraia mara nyingi lakini mwisho wa siku sisi wasanii tunajiingiza kwenye maswali mazito sana na yanahitaji kutafakari zaidi na mimi siamini kwamba lazima uwe na passport ya nchi fulani na sasa hivi naona watu wengine wanaanza kuelewa hilo,” alisema.

“Nchi nyingi sana wanakubali uraia wa nchi mbili, hata Denmark juzi wamekubali. Mali wamekubali, Kenya wamekubali na watu wakijieleza wana shida gani wanasikilizwa na kusaidiwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents