Habari

Na mimi nataka kusifiwa nikiwa hai, mtu anasema yupo kwenye foleni kumbe analiwa – Rais Magufuli (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanasiasa wa upinzani na Watanzania kwa ujumla wampongeze pale panapo bidi na sio kila kitu kukosoa na kushindwa kuona mazuri anayoyafanya.

Rais Magufuli amesema hayo leo Desemba 18, 2018 alivyokuwa anahutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa Barabara ya Kimara-Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2.

Mnapata vigugumizi gani kusema Rais unasimamia vizuri kodi? Mtu anasema hiyo barabara ni kodi zetu, ni kweli, lakini kwani kodi mmeanza kulipa leo? Mbona hazikuwa zinajenga barabara? Si mnipongeze nasimamia kodi vizuri. Na mimi nataka kusifiwa nikiwa hai,” amesema Rais Dkt Magufuli .

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema kuwa ujenzi huo wa barabara utasaidia kupunguza foleni, jambo ambalo limekuwa likivunja ndoa nyingi kwenye jamii.

Zipo ndoa zimevunjika kwa sababu ya msongamano wa barabara hii, mtu anatumia sababu za msongamano huu, anarudi nyumbani usiku. Anasema barabara msongamano magari ni shida, kumbe jamaa analiwa. Sio kuliwa kule mnakojua nyie wenyewe!!“amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara – Kibaha kwa urefu wa kilometa 19.2, upanuzi wake utakuwa wa njia 6 hadi 8.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents