Burudani

Naanza muziki upya na Spidoch Band – Beka

Msanii wa muziki, Beka Ibrozama, ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Tumaini’, amejipanga na ujio wa bendi yake mpya iitwayo ‘Spidoch Band’.

Muimbaji huyo alikuwa kimya kwa kipindi cha miaka 3 akiandaa bendi yake hiyo, ambayo itazinduliwa Aprili 29 katika ukumbi wa Next Door, Masaki Jijini Dar es salaam.

Akiongea na Bongo5 kuhusu ujio huo, Beka amedai alipokuwa nje ya muziki alipata nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitaboresha style ya muziki wake.

“ Mimi Beka nimerudi upya kwenye muziki,tena kwa miguu miwili. Nimejifunza vingi, na kubwa zaidi ni ujio wa bendi yangu mpya, ambayo nitaizindua hivi karibuni. Ni bendi ya muziki ambayo inaendana na hadhi ya kimataifa kwa hiyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya muziki mzuri,” alisema Beka.

Beka amesema alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda wake wote kwaajili ya kuandaa bendi yake na kwa sasa amerudi rasmi na kilichobaki ni mashabiki zake wasubiri kupata mziki mzuri kutoka kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents