Burudani

Nacha amtaja Bonta kuhusika katika ‘Boss Mpya’

Baada ya kuachia ngoma yake mpya ya ‘Boss Mpya’ rappar Nacha anayechipukia katika game ya muziki amefunguka juu ya msanii Bonta, kuhusika katika ngoma hiyo aliyofanya na G-Nako.

Akipiga stori katika Stardand Mix ya Stardand Fm, mkali huyo amemuambia mtangazi Emmanuel Mlelekwa kuwa idea ya wimbo alikuwa nayo yeye ila jina la ngoma hiyo ametoa Bonta kutoka kundi la Weusi.

“Kwanza mie ni apply kuwa ni shabiki mkubwa ya Gnako, hii ngoma ajue amefanya na shabiki yake , kilichokuja kutojkea kwanza mimi nina mahusiano mazuri na Bonta ambaye ni memba wa Weusi, mtu ambaye yupo nyuma ya ngoma hii ni Bonta ambaye amechukua Gnako na mimi then tukaingia studio kufanya kitu kimoja, ” amesimulia Nacha.

Pia Nacha aliongeza kuwa idea ya ngoma hiyo ni yake ila jina la wimbo alikitoka kwa rapper Bonta ambaye kwa sasa ana hit na ‘Zero’ aliyomshirikisha Barakah The Prince.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents