Michezo

Nacheza Chelsea ila ni shabiki wa Madrid – Morata

Straika wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata anaamini iposikumoja atarejea tena katika timu yake ya zamani ya Real Madrid.

Straika wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata

Morata mwenye umri wa miaka 23, yupo katika majuku na timu yake ya taifa ya Hispania inayotarajia kucheza michezo ya kirafiki dhidi ya Costa Rica na Urusi amesajiliwa na klabu ya Chelsea kwa dau la paundi milioni 70.

“Bilashaka ningelipenda siku moja nirejee tena Real Madrid ijapokuwa nafahamu si kazi rahisi.” Morata ameiambia radio Cadena Ser kwenye kipindi chao cha El Larguero nchini Hispania.

Morata ameongeza “Nilimuambia kocha nahitaji kucheza zaidi hasa katika hatua ya mtoano ya klabu bingwa barani Ulaya.”

“Sikuwahi kuizungumzia vibaya Real siku zote nitasema kuwa ni klabu bora zaidi kwangu mimi, licha ya kuichezea Chelsea ila nishabiki wa Madrid.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents