Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Nadal atwaa taji la US Open

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora, Rafael Nadal ametwaa taji la michuano ya wazi ya Marekani ‘US Open’ baada ya kumshinda mpinzani wake, Kevin Anderson hapo jana siku ya Jumapili.

Rafael Nadal atwaa taji lake la tatu la US Open kwa ushindi wa  6-3 6-3 6-4 dhidi ya Kevin Anderson

Nadal maarufu kama “The King of Clay” ameshinda taji lake hilo la 16 la Grand Slam huku ikiwa ni la tatu kwa mashindano ya US Open baada ya kumshinda mpinzani wake kwa seti 6-3 6-3 6-4 katika mchezo wa fainali uliyochezwa katika viunga vya Arthur Ashe Stadium.

Mzaliwa huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 31, Rafael Nadal Parera hilo ni taji lake la pili kubwa kunyakuwa mwaka huu baada ya kuanza na lile la French Open mwezi Juni.

Mara baada ya ushindi huo Nadal amesema kuwa wiki mbili hizi zimekuwa ni maalumu kwake.

“Bila shaka wiki mbili hizi zimekuwa maalumu kwangu, nashindwa kuamini kwa kile kilichotokea mwaka huu baada ya kupita miaka mingi nikisumbuliwa na matatizo mbalimbali, majeraha na hata kutocheza vizuri,”. Nadal amekiambia chombo cha habari cha Sky Sport.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW