Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nadya amrithi Nancy Kinondoni

Nadia MWANADADA Nadya Mohammed, juzi alitwaa taji la ‘Giraffe Ocean View Miss Kinondoni 2006’ baada ya kuibuka malikia wa kanda hiyo kwa kuwashinda wenzake 13 katika shindano lililofanyika..

Nadia Mohamed akivishwa taji na Nancy Sumari
Nadia Mohamed akivishwa taji na Nancy Sumari

MWANADADA Nadya Mohammed, juzi alitwaa taji la ‘Giraffe Ocean View Miss Kinondoni 2006′ baada ya kuibuka malikia wa kanda hiyo kwa kuwashinda wenzake 13 katika shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Mlimbwende huyo aliyerithi mikoba ya Nancy Sumari, alizawadiwa gari aina ya Mitsubishi Lancer lenye thamani ya sh mil. 8 na ataungana na Hawa Sepetu na Sophia Kapama kwenye kambi ya Vodacom Miss Tanzania.

Nancy ambaye kwa sasa ni mrembo wa Dunia, Kanda ya Afrika aliibuliwa Kinondoni na kufanya vema kwenye Miss Tanzania. Katika shindano la Dunia, alikuwa mmoja wa warembo sita bora walioingia fainali.

Hawa aliyeshika nafasi ya pili, atazawadiwa sh 800,000 wakati Sophia aliyeshika nafasi ya tatu atazawadiwa sh 500,000. Mshindi wa nne, alikuwa Christabelle Peter atakayepata sh 300,000 na mshindi wa tano ni Nadya Ahmed atapata sh 200,000.

Nadia Mohamed -C, Wema Sepetu -L na Sophia Kapama -R,
Nadia Mohamed -C, Wema Sepetu -L na Sophia Kapama -R

Warembo wengine walioingia katika kumi bora ni Tina Ambrose, Vivian Sirikwa, Grace Gabriel, Yvone Mashuda na Ania Said ambao kila mmoja atapewa sh 100,000 na waliobaki Harieth Kibambe, Ngehu Jackson, Joy Mzava, Judith Mushi kila mmoja atapata kifuta jasho cha sh 50,000.

Kadhalika Ngehu aliibuka kuwa kimwana mwenye kipaji baada ya kuimba vema wimbo wa kundi la Makoma wakati Christebella alishinda taji la vazi bora la ubunifu na wakati kinara wa shindano hilo, Nadya pia alishinda taji la mrembo mwenye haiba na muonekano mzuri katika picha ‘Photogenic’.

Shindano hilo limedhaminiwa na Photo Point, Shear Illisions, Vodacom, Nakiete Pharmacy, Giraffe Ocean View, Redds’, 88.4 Clouds FM, G Class Saloon, MayFair Plaza Mikocheni, CxC Holdings & Safaris Tour, Hoteli ya Regency, Screen Masters, AJIM Enterprises na Executive Solutions iliyotangaza kutoa ajira kwa warembo watano pamoja na fedha sh 800,000 kwa warembo hao.

Shindano hilo lilipambwa na bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wajelajela Gwa’ au Wazee wa Gwasuma.

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW