Michezo

Nafasi ya Tanzania ni ipi AFCON 2019 Misri, baada ya kupangiwa timu hizi

Hatimaye makundi sita ya mchuano wa Kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2019 yamepangwa. Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwa vyoyote vile habari kubwa kwa sasa ni Kundi C ambalo linaundwa na mataifa jirani ya Kenya na Tanzania.

Mataifa hayo, yanaungana pamoja na vigogo wa mpira wa Afrika mataifa ya Senegal na Algeria.

Kwa upande wa Uganda wao wapo Kundi A pamoja na wenyeji Misri, DR Congo na Zimbabwe.

Burundi wapo kwenye Kundi B pamoja na Nigeria, Madagascar na Guinea.

https://twitter.com/CAF_Online/status/1116791311472836608/photo/1?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1116791311472836608&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.bbc.com%2Fswahili%2Flive%2Fmichezo-47905605

    • Kundi F
      • Cameroon,
      • Ghana,
      • Benin,
      • Guinea-Bissau
      Article share tools
    • Imepakiwa mnamo 22:59 12 Apr22:59 12 AprKundi E
      • Tunisia
      • Mali
      • Mauritania
      • Angola
      Article share tools
    • Imepakiwa mnamo 22:57 12 Apr22:57 12 AprKundi D
      • Morocco,
      • Ivory Coast,
      • South Africa,
      • Namibia
      Article share tools
    • Imepakiwa mnamo 22:54 12 Apr22:54 12 AprKundi C
      • Senegal
      • Algeria
      • Kenya
      • Tanzania
      Article share tools
    • Imepakiwa mnamo 22:53 12 Apr22:53 12 AprKundi B
      • Nigeria
      • Guinea
      • Madagascar
      • Burundi
      Article share tools
    • Imepakiwa mnamo 22:46 12 Apr22:46 12 AprKundi A
      • Misri
      • DRC
      • Uganda
      • Zimbabwe
      Article share tools

Kwa mujibu wa BBC, kuwa ilitangazwa kuwa droo hiyo itapangwa saa 3 usiku kwa saa za Afrika lakini mpaka baada ya saa moja na nusu baadae, bado droo ilikuwa haija pangwa. Hali hiyo imeoneka pia kuwaudhi baadhi ya watu.

https://twitter.com/CAF_Online/status/1116770724633620486/photo/1?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1116770724633620486&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.bbc.com%2Fswahili%2Flive%2Fmichezo-47905605

Harambee Stars ya Kenya kuzawadiwa ksh.250,000 kwa kila ushindi AFCON

Burundi yafuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza

Burundi ilifuzu katika kombe la mataifa ya Africa AFCON kwa mara ya kwanza baada ya kumzuia mshambuliaji wa Gabon na Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang wakitafuta droo ya 1-1.

Huku Burundi ikihitaji droo ya 1-1, wageni Gabon walioandaa fainali za kombe la 2017, walihitaji kupata ushindi ili kujiunga na washindi wa kundi C Mali katika kinyang’anyiro hicho kilichopanuliwa na kushirikisha timu 24 nchini Misri kuanzia mwezi Juni na Julai.

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City nchini Uingereza Saido Berahino aliiongoza miamba hiyo ya Afrika mashariki.

Burundi inajiunga na Madagascar pamoja na Mauritania miongoni mwa mataifa yatakayoshiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza huku ufanisi wao ukizua sherehe katika taifa hilo.

Katika kipindi chote cha mechi hiyo Burundi ilizuiliwa na kipa wa siku nyingi wa Gabon Didier Ovono kabla ya Cedric Amissi kufunga bao la pekee dakika ya 75.

Hatahivyo sherehe hizo zilizuiliwa hadi katika kipenga cha mwisho wakati Gabon ilipofuzu baada ya beki wa Burundi kujifunga.

Mshambuliaji wa Stoke City Saido Berahino

Nyota wa kandanda wamiminika Misri

Mambo yameiva nchini Misri na muda wowote kutoka sasa droo itaanza kupangwa.

Wachezaji nyota wa zamani barani Afrika wakiongozwa na Yaya Toure, Didier Drogba, Elhadji Diouf na Mustafa Hajd wote wamefika katika ukumbi itakapofanyika shughuli hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano ya Afcon kuongezwa idadi ya timu shiriki toka 16 mpaka 24.

Kocha wa Tanzania ‘aongea kiarabu’

Emmanuel Amunike ni moja ya wachezaji maarufu wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria.

Ameongeza umaarufu wake barani Afrika baada ya kuipeleka Tanzania kwenye michuano ya Afcon baada ya makocha wengine kushindwa kwa miaka 39.

Lakini je unajuwa gwiji huyo anaambulia lugha ya kiarabu?

Michuano ya Afcon ya mwaka huu inafanyikia Misri, na Amunike alishawahi kuishi nchini humo toka mwaka 1991 mpaka 1994 akichezea klabu kongwe ya Zamalek.

Mtizame mwenyewe kwenye video hiyo chini ‘akimwaga’ kiarabu.

Uganda yafuzu mara ya pili mfululizo

Tofauti na Tanzania ambao walitupwa nje kwa miaka 39, Kenya waliosubiri kwa miaka 15 ama Burundi ambao wamefuzu kwa mara ya kwanza, hii ni mara ya pili mfululizo kwa Uganda kushiriki michuano ya Afcon.

Uganda walishiriki michuano hiyo miaka miwili iliyopita (2017) nchini Gabon na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Kabla ya 2017, Uganda nao walisubirikwa miongo mitatu kufuzu.

Uganda ilifuzu katika nafasi ya kwanza kwenye kundi L ikufuatiwa na Tanzania katika nafasi ya pili.

Kwa maoni yako timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars unaipa nafasi ipi katika kundi lao C ambalo lina timu kama Senegal, Algeria, Kenya na Tanzania yenyewe…? lakini pia unahisi timu gani itaibuka kidedea na kuwa bingwa katika michuano hii…?

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents