Michezo

Nahodha sio tu kuvaa kitambaa, Mwanjale anakubalika – Manara (Video)

Mkuu wa idara ya habari wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kuwa maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Joseph Omog kumvua unahodha mchezaji, Jonas Mkude yapo sahihi.

Mkuu wa idara ya habari wa klabu ya Simba, Haji Manara

“Mwanjale ameshakuwa nahodha wa timu ya taifa ya Zimbabwe ameshakuwa nahodha wa Power dynamo ambayo imecheza nusu fainali ya klabu bingwa Afrika, lakini ni mchezaji anayekubalika sana ndani ya timu yenyewe na anauzoefu mkubwa”.Amesema Haji Manara ambaye ni mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC

Manara ameongeza kuwa “Bocco hivyo hivyo ameshawahi kuwa nahodha wa Azam FC na walikuwa pamoja na kocha Omog hivyo anamjua vizuri na anaona muunganiko huu utakuwa na manufaa, unahodha sio tu kuvaa kitambaa lakini katika vyumba vya kubadilishia nguo huwa ana nafasi kubwa sana ambayo watu wengi wamekuwa hawaelewi”.

“Simba si mara ya kwanza kubadilisha nahodha kabla ya Mkude alikuwa Cholo na alivyo kabidhiwa yeye kitambaa cha unahodha hapakuwa na tatizo lolote na timu inaendelea vizuri tu”.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents