Michezo

Nahodha wa JKU ataka kupongezwa kwa kufungwa goli 7 na Zesco

Baada ya wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika JKU na Zimamoto kutolewa katika hatua za awali za mashindano hayo mwanzoni mwa juma hili, hatimaye nahodha wa mabingwa wa tetezi wa kombe la visiwani humo, Issa Haidary Alawi amejitokeza na kuhitaji  kupongezwa kwa timu yake kufungwa jumla ya mabao saba mbele ya Zesco ya Zambia.

Issa Haidary Alawi amesema kuwa timu yake ya JKU kukubali kipigo cha mabao 7 – 0 dhidi ya Zesco ya Zambia ili stahili na hivyo wanahitaji pongezi maana wangefungwa mengi zaidi ya hayo.

Hao Zesco ni zaidi yetu sisi au ni zaidi ya watu wengine kwa sababu hata uwanjani walikuwa wanadiriki kutuambia waarabu sisi tunawakalisha hapa tunawafunga waarabu.

Sasa sisi tunajilinganisha na waarabu inakuwaje, kwahiyo nafikiria kwa matokeo yale pale watu watupongeze sana hadi magoli kufikia kuwa vile.

Kwa upande wa katibu Mkuu wa JKU, Saadu Maalim Ujudi amesema kuwa wamejifunza maana ya kucheza nyumbani na ugenini kwakuwa wapinzani wao walikuwa na mbinu za kila haina.

Ni matokeo ya mpira kutokana na hali ya hewa na mbinu za kila haina kuna ujanja ambao ulifanyika kule tulikuwa tumeuwona si wenyewe jinsi gani ulivyotokezea.

Katika kombe la Klabu Bingwa JKU wamefungwa na Wenyeji Zesco ya Zambia mabao 7-0 na kufanya kutelewa kwa jumla ya mabao 7-0 kufuatia mchezo wa awali uliochezwa Amaan Zanzibar kumalizika kwa sare ya 0-0.

Wakati Zimamoto ambao walikuwa wanawakilisha Zanzibar katika Kombe la Shirikisho nao wametolewa kwa kufungwa 1-0 na wenyeji wao Wallaita Dicha ya Ethiopia na kufanya watolewe kwa jumla ya mabao 2-1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents