BurudaniVideos

Nahofia kutoa nguo za PKP sababu watu hawachelewi kutoa feki na kupiga hela – Ommy Dimpoz (Video)

Ommy Dimpoz amesema anahofia kutoa nguo zake za PKP kwasababu amegundua kuwa kuna watu wanaotengeneza nguo feki za brands zingine za Kitanzania na kuziuza kwa bei chee.

13118112_615300868638474_172335028_n

Amesema bado anafikiria njia nzuri za kuweza kuhakikisha hakuna wajanja wataoweza kula kupitia brand yake. “Sijajua wenzangu wanazifanya kwa style ipi lakini bado kuna tatizo la watu kutumia brand za watu wengine kufyatua,” Ommy aliiambia Bongo5.

Amesema ameshahudia mtu kuulizia kofia za rafiki yake ambaye huziuza kwa shilingi elfu thelathini lakini akawaambia Kariakoo zinauzwa kwa elfu kumi tu.

“Kweli kwenda kufuatilia akakuta kuna watu wanatengeneza nyingi. Kwahiyo najaribu kufikia kwamba nitafanyaje biashara nisitumie nguvu yangu kupromote halafu mwingine aende kupata kiulaini,” ameongeza.

Wasanii ambao tayari wameingiza bidhaa za brand zao ni Jux mwenye African Boy, Weusi, Tip Top Connection na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents