Habari

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson atangaza kugombea ubunge 2020. Je, atagombea Mbeya Mjini avaane na Sugu? mwenyewe ajibu

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameweka wazi kuwa mwaka 2020 atagombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Sugu na Dkt. Tulia Ackson

Dkt. Tulia ameweka wazi mipango hiyo leo Agosti 19, 2019 kwenye mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio, Ambapo amesema anaamini yeye ni mchapakazi na ndio maana amekuwa akiteuliwa katika nyadhifa mbalimbali.

Kuhusu watu wanaosema kuwa mimi mafanikio yangu yamekuwa ya haraka sana, hilo kuna watu wa kulizungumzia nataka kuamini watu ambao wamekuwa wakiniteua itakuwa wameona kazi niliyokuwa nikiifanya.“ameongea Dkt. Tulia na kuweka wazi malengo yake ya kugombea Ubunge mwakani.

Mwenyezi Mungu akitupa Uhai 2020 nitagombea, ila nitagombea wapi? naomba watulie kwa sababu chama chetu kina utaratibu wake ila nashukuru ninavyoonekana nina uwezo wa kugombea maeneo mengi.“amesema Dkt. Tulia.

Tangu mwaka jana kumekuwa na tetesi kuwa Dkt. Tulia atagombea jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu mwakani. Jimbo hilo kwa sasa lipo chini ya CHADEMA na linaongozwa na Mhe. Sugu.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents