Burudani ya Michezo Live

Naibu Waziri Masauni ahoji tsh milioni 840 kutumika kulisha wafungwa

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Magereza mkoani Arusha, kujitahmini na kujirekebisha baada ya kuzalisha kiasi kidogo cha mahindi na maharage, hali inayopelekea Serikali kuendelea kutumia kiasi kikubwa cha fedha kununua chakula cha wafungwa

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni

Masauni ameyasema hayo alipotembelea Gereza Kuu la Arusha, ambalo ni moja kati ya Magereza kumi ya kimkakati nchini, yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt John Magufuli la kutaka jeshi hilo lijitegemee kwa chakula kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa na ardhi waliyonayo badala ya kutegemea bajeti kutoka serikalini.

“Gharama za kununua magunia 3,500 ya Mahindi na Maharage, utakuwa unahitaji zaidi ya milioni 840 fedha ambazo zinaweza kutumika kulisha wafungwa, hoja ya ukame sioni kama ni ya msingi, wakati kuna mifumo ya umwagiliaji ambayo gharama zake hazizidi milioni 326, kwahiyo mmeshindwa kutumia milioni 326 kwa mara moja ili kuokoa milioni 840 kwa kila mwaka” amesema Waziri Masauni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW