Habari

Naibu Waziri wa afya awataka watoto kutambua haki na wajibu wao

Watoto wa Tanzania wamehamasishwa kutambua Haki na wajibu wao katika jamii kwa kuhakikisha wanazijua na kuzidai haki zao za msingi na kutimiza wajibu wao kama watoto katika jamii.

Hamasa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la Watoto wa Mkoani Shinyanga na kuzindua rasmi Baraza hilo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa watoto wanatakiwa wasikae kimya pale wanapoona haki zo hazitimizwi bali wachukue hatua ya kutoa taarifa katika ngazi husika ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wanaowanyima watoto haki zao.

Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amezianisha Haki za Mtoto kuwa ni Haki ya Kuishi, kuendelezwa, Kulindwa, Kushirikishwa na Kutobaguliwa.

Ameongeza kuwa Mabaraza ya watoto yana umuhimu mkubwa katika kuwajenga watoto katika maadili mema na kuijenga jamii ijayo hivyo Mikoa na Halmashauri hazina budi kuyalea na kuyasimamia mabaraza hayo kwa mstakabali wa maendeleo ya Mtoto na taifa.

Amesisitiza kuwa Mabaraza hayo pia yanaweza kutumika kama sehemu muhimu ya kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa mimba na ndoa za utotoni ambavyo vinawakumba sana watoto.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii anayeshughulikia masuala ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mathias Haule amesema kuwa mabaraza ya watoto yanatoa fursa kwa watoto kujadili agenda zao na kuwasilisha maoni yao kwenye mamlaka husika ili kuhakikisha kuwa kuzingatia mahitaji ya watoto yanazingatiwa katika mipango, Sera, na maamuzi mbalimbali.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela amehaidi kushirikiana na Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii katika kuyaleta na kuyapa mwongozo Mabaraza ya watoto ili yaweze kuleta tija katika makuzi ya watoto na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents