Habari

Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ataka studio ya mastering ianze kazi

Naibu Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala ametaka kuanza kufanya kazi mara moja kwa mastering studio iliyokabidhiwa kwa wasanii nchini mwaka 2006 na rais Jakaya Kikwete.

Akiongea na umoja wa wasanii ujulikanao kama Tanzania Flava Unit, TFU, alipotembelea ofisi za Tanzania House of Talents, THT, ili kupata maelezo ya sababu za kushindwa kufanya kazi kwa studio hiyo, naibu waziri Makala alisema studio hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa faida ya wasanii wote kama alivyokusudia rais Kikwete.

“Maneno haya yanakuja kwasababu studio haifahamiki. Mimi nataka kuona kwamba nia nzuri ya rais inatumiwa,” alisema.
Aliongeza kuwa serikali haitokaa kimya kuhusiana na mgogoro uliopo wa studio hiyo baina ya wasanii.

Pia mheshimiwa Makala ameutaka uongozi huo wa TFU kupeleka vifaa hivyo vya studio ya mastering ofisini kwake October 2 mwaka huu ili avione.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents