Habari

Nairobi: Aliyenusurika shambulio la Septemba 11 Marekani ni miongoni mwa waliouawa

Aliyenusurika katika shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 ni miongoni mwa watu 14 waliouawa na magaidi kwenye jengo lenye hoteli ya Dusit 2, Riverside jijini Nairobi nchini Kenya.

Kijana huyo Mfanyabiashara raia wa Marekani, anajulikana kwa jina la Jason Spindler ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya I-Dev International, alinusurika katika shambulizi lililofanywa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda likiongozwa na Osama Bin Laden, baada ya ndege zilizotekwa kugongeshwa kwa makusudi kwenye majengo mawili jijini Washington DC na New York ambapo watu 3,000 walipoteza maisha.

Mama yake Spindler ameliambia Shirika la Habari la NBC kuwa wamesikitika kumpoteza kijana wao ambaye alikuwa na umri mdogo.

Taarifa ya kitengo cha Ubalozi wa Marekani nchini Kenya kimethibitisha kuwa raia wa Marekani ni mmoja kati ya watu waliouawa kwenye shambulizi hilo la Nairobi lakini haitoa taarifa zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents