Habari

Naisihi serikali itazame jambo la Kibiti kwa mtazamo mpana – Mhe. Zitto

Baada ya usiku wa kuamkia leo Afisa Mtendaji kijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake wameuwawa kwa risasi katika kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti. Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameisihi itazame jambo hili kwa mtazamo mpana na wenye weledi.

Mhe. Zitto ameyaanisha hayo leo katika ukurasa wake wa Facebook huku akisema kuwa wananchi wanahaki ya kujua nini kinaendelea huko.

Mauaji mengine Kibiti! Usiku wa kuamkia leo Afisa Mtendaji kijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake wameuwawa kwa risasi na baadaye kuchoma moto nyumba.
Naisihi Serikali itazame jambo hili la MKIRU ( Mkuranga, Kibiti na Rufiji) Kwa mtazamo mpana na wenye weledi. Tambo za IGP na Amiri Jeshi Mkuu zinaonekana ni maneno matupu. Wananchi wana haki ya kujua nini kinaendelea MKIRU.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents