Burudani

Nakaaya aula Tusker Project Fame

NakaayaMSANII wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari ndiye atakayewafundisha washiriki wa shindano la kuvumbua vipaji la Tusker Project Fame linalotarajiwa kuanza Machi mosi. Shindano hilo litachukua wiki kumi na litashirikisha washiriki 15 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda na litafanyika nchini.

NakaayaDeus Gabone

 

 

 

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari ndiye atakayewafundisha washiriki wa shindano la kuvumbua vipaji la Tusker Project Fame linalotarajiwa kuanza Machi mosi.

 

 

 

Shindano hilo litachukua wiki kumi na litashirikisha washiriki 15 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda na litafanyika nchini.

 

 

 

Nakaaya ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Mr. Politician ni miongoni mwa wasanii walioibuliwa na shindano hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini Kenya mwaka jana.

 

 

 

Katika shindano hilo, Nakaaya alitolewa wiki ya tano ya mashindano hayo yaliyodumu kwa wiki saba.

 

 

 

Akizungumza na safu hii Nakaaya alisema anafurahi kupata nafasi hiyo na kuongeza kuwa ataitumia vizuri kuwaelekeza washiriki kuonyesha vipaji vyao.

 

 

 

Tayari msanii huyo ameshakamilisha albam yake yenye nyimbo kumi na ameshaiingiza sokoni takriban wiki mbili zilizopita.

 

 

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents